Yanga ikifanya haya wanampiga Mwarabu kweupe

Dar es Salaam. Kocha wa zamani wa Stand United, Athuman Bilali 'Bilo' amesema ili Yanga itoka kifua mbele dhidi ya Pyramid FC wanayocheza nayo Oktoba 27, wachezaji wanatakiwa kujengewa uzalendo.

Bilo alisema uzalendo umebeba kujitolea kwa hali na mali, jambo analoliamini mastaa wa Yanga wakijengewa basi watafanya maajabu katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inacheza Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa na Zesco ya Zambia kwa mabao 2-1 ugenini.

"Naamini Yanga wanaweza wakufanya maajabu wachezaji wenyewe waamue kufanya kitu cha tofauti katika mchezo huo, uzalendo ukikaa akilini na mioyoni mwao kwamba ndio timu pekee inayowakilisha nchi basi watapata ushindi."

"Kitu chochote ukifanya ukiona watu hawakuamini basi unatakiwa kuwaonyesha kwa matendo ili wanyamaze ndicho wanachotakiwa kufanya wachezaji wa Yanga kwani kwa mwenendo wao wanaonekana hawawezi kufanya lolote,"alisema Bilo.