Yanga kuivaa JKT Tanzania bila Makambo

Saturday February 9 2019

 

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga Heritier Makambo kesho Jumapili atakosekana  kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachomenyana na JKT Tanzania Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Makambo ataukosa mchezo huo utakaopigwa Mkwakwani mkoani Tanga kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kadi ya tatukwa Makambo ilitolewa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati timu hizo zilipokutana na matokeo kumalizika kwa timu hizo bila kufangana.

Hadi sasa Makambo amefikisha mabao 11 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara  akiongoza huku akifuatiwa na  Said Dilunga mwenye mabao 10 sawa na Eliud Ambokile.

Mechi zingine ambazo zitachezwa Jumatatu ni Mwadui watakutana na Mtibwa, African Lyon watamenyana na Ruvu Shooting, Mbao FC watawakaribisha Coastal Union, Prisons watakuwa na kibarua cha kuendeleza heshima yao wakiwakaribisha Stand United.

Pia mechi zingine zitawakutanisha KMC dhidi ya Alliance, huku Ndanda FC watakuwa wakiwakaribisha Kagera Sugar.  Lipuli watacheza dhidi ya Azam FC.

Advertisement