Yanga kutikisa Kigoma leo

Yanga  leo Ijumaa jioni  itaikabili Mgongo Fc inayoshiriki Ligi Daraja la pili  kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.
Baada ya mchezo huo pia Yanga itacheza na  Jumapili   na michezo yote itakuwa maalumu kwtimu hiyo kujiwinda dhidi ya Iringa United watakayokutana nayo Desemba 23 kwenye  kombe la Shirikisho (FA).
Kocha msaidizi wa Yanga Said Maulid 'SMG', alisema wanakwenda kutumia michezo hiyo miwili kama sehemu ya kuangalia makosa na ubora uliokuwa katika kikosi chao kabla ya kucheza mechi ya FA pamoja na zile za Ligi Kuu Bara.
Maulid wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wasiokuwa na majukumu ya timu ya taifa wapo katika ziara hiyo ya Kigoma isipokuwa wacheza wa kigeni pekee ndio hawajaambatana na timu hiyo.
 "Tumewaacha Dar es Salaam,  Kabamba Tshishimbi, David Molinga na Patrick Sibomana, ambao walitakiwa kwenda nchini kwao kwa mapumziko ya wiki moja lakini baada ya kushindikana hilo na umuhimu wa mechi hizi mbili wanatakiwa kujiunga mapema na wenzao ili kuendelea na maandalizi," alisema.
"Tupo katika wakati wa kufanya maandalizi sahihi ya kujiandaa na mechi ngumu zilizokuwa mbele yetu ndio maana tumezichukulia mechi hizi katika umuhimu wa hali ya juu kwani mbali ya matokeo tunataka kuona vile ambavyo tumevifanyia kazi mazoezini.
"Tunaomba mashabiki wote wa Yanga katika mkoa wa Kigoma wajitokeze kwa wingi uwanjani kwani mbali ya mchezo mzuri ambao watauona pia  tutawapa burudani  pamoja na  ushindi," alisema Maulid ambaye pia aliwahi kuwa  mchezaji wa  kikosi hicho miaka ya nyuma"alisema Maulid