Yanga yapangua ratiba Ligi Kuu Tanzania kisa Waarabu

Muktasari:

  • Yanga ina kibarua kigumu Oktoba 27 dhidi ya Pyramid katika Kombe la Shirikisho Afrika mchezo ambao wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Dar es Salaam .Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mbao dhidi ya Yanga uliokuwa uchezwe Oktoba 24 umerejeshwa nyuma na sasa utachezwa Oktoba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kupitia katika akaunti rasmi ya klabu Yanga walitangaza mchezo wao dhidi ya Mbao umerejeshwa nyuma huku wakiwa hawajaweka sababu rasmi ya mchezo huo kupigwa tarehe hiyo.
Taarifa zinadai kuwa sababu kubwa ya mchezo kurejeshwa nyuma ni Yanga kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika watakaocheza na Pyramid mkoani humo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Yanga ina kibarua kigumu Oktoba 27 dhidi ya Pyramid katika Kombe la Shirikisho Afrika wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Klabu hii iliamua kuhamishia mechi yao na Pyramid mkoani Mwanza kutokana na kuwa na mchezo wa Ligi Kuu mkoani humo.