Yanga yatupwa Misri kwa Pyramids Kombe la Shirikisho Afrika

Dar es Salaam. Yanga imepangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC ya Misri katika mechi ya kusaka kufuzu kwa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.

Katika ratiba hiyo ya CAF, Yanga ilipangwa Chungu A sasa watakutana na Pyramids FC timu iliyoanzishwa mwaka 2008, inashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Yanga itaanza mechi yake ya kwanza nyumbani Oktoba 27, 2019 kabla ya kurudiana Misri itakuwa Novemba 3, 2019 mshindi wa mchezo huo anafuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi.

Pyramids FC inafundishwa na kocha wa zamani wa Uganda, Mfaransa Sebastien Desabre ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuiing’oa Belouizdad katika raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1.

Kocha wa Pyramids FC, Desabre amesema kikosi chake ni Paris Saint Germain (PSG) ya Afrika.

Desabre alichukua jukumu la kuinoa Pyramids FC Julai baada ya kuachana na Uganda kufuatia kuondolewa mapema katika fainali za Mataifa ya Afrika Misri 2019.

Michezo mingine ya hatua hiyo ya mtoano itashuhudia Horoya AC ya Guinea watakuwa na kibarua dhidi ya Bandari ya Kenya, Enyimba (Nigeria) watakuwa wenyeji wa TS Galaxy (Afrika Kusini).

Asante Kototo (Ghana) itacheza dhidi ya FC San Pedro (Ivory Coast), huku Gor Mahia (Kenya) itawakaribisha DC Motema Pembe (DR Congo), UD Songo ya Msumbiji itaivaa Bidvest Wits (Afrika Kusini).

Ratiba kamili

Horoya (Guinea) vs Bandari (Kenya)

Young Africans (Tanzania) vs Pyramids (Egypt)

Enyimba (Nigeria) vs TS Galaxy (South Africa)

Zamalek (Egypt)/Generation Foot (Senegal) vs ESAE (Benin)

Asante Kotoko vs San Pedro (Cote d'Ivoire)

KCCA (Uganda) vs Paradou (Algeria)

Gor Mahia (Kenya) vs DC Motema Pembe (DR Congo)

UD Songo (Mozambique) vs Bidvest Wits (South Africa)

Elect Sport (Chad) vs Djoliba (Mali)

Green Eagles (Zambia) vs HUSA (Morocco)

Cano Sports (Equatorial Guinea) vs Zanaco (Zambia)

Fosa Juniors (Madagascar) vs RS Berkane (Morocco)

Cote d'Or (Seychelles) vs Al Masry (Egypt)

ASC Kara (Togo) vs Rangers (Nigeria)

FC Nouadhibou (Mauritania) vs Triangle United (Zimbabwe)

El Nasr (Libya) vs Proline (Uganda)