VIDEO: Yanga yawatambulisha Bumbuli, Nugaz nafasi zao zaleta mjadala

Muktasari:

Hassan Bumbuli anakuwa Afisa Habari Mkuu wa Yanga huku Antonio Nugaz akiwa Afisa Mhamasishaji mkuu.

Khatimu Naheka

Dar es Salaam. Uongozi wa Yanga umewatambulisha rasmi Afisa Habari Mkuu, Hassan Bumbuli na Afisa Mhamasishaji Mkuu, Antonio Nugaz.

Aliyewatambulisha wawili hao ni kaimu katibu mkuu Dismas Ten aliyekuwa Afisa Habari Mkuu.

Ten amesema viongozi hao sasa wanakuwa familia ya Wanayanga wakisaidiana na uongozi wa klabu hiyo kuendeleza kwa kasi malengo ya klabu hiyo.

Hata hivyo katika mkutano huo utata wa utofauti wa majukumu yao uliibuka kwa wanahabari kuhoji jinsi watakavyokuwa wakifanya majukumu yao.

Ten alifafanua kuwa ingawa ni nafasi mbili tofauti, lakini majukumu yao watakuwa yakifanyika kwa ushirikiano.

Ten alisema Bumbuli ndiyo atakuwa bosi mkuu wa mambo ya habari naawasiliano, pia kwa atakayekuwasiliana na Nugaz kama atakuwa na taarifa katika suala la atakaloulizwa anaweza kulitolea ufafanuzi.