Zaha, Bony aibeba Ivory Coast Afcon Misri

Muktasari:

  • Ivory Coast imepangwa kundi la kifo katika AFCON ikiwa pamoja na Morocco, Afrika Kusini na Namibia.

Cairo, Misri. Kocha wa Ivory Coast, Ibrahim Kamara ameita wachezaji 23, tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika zitakazoanza Juni 21- Julai 19, Misri.

Ivory Coast imepangwa kundi la kifo katika AFCON ikiwa pamoja na Morocco, Afrika Kusini na Namibia.

Kamara ametangaza kikosi cha mwisho kutoka kile cha wachezaji 28 baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Comoros Ijumaa iliyopita.

Kikosi cha Tembo hao kinawategemea Nicolas Pepe,  winga Crystal Palace, Wilfried Zaha. Mkongwe Wilfried Bony, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Qatari katika klabu ya Al Arabi, pia yupo kiungo wa Milan, Franck Kessie.

Hata hivyo, winga wa zamani wa Arsenal na Roma, Gervinho ameachwa pamoja na kuwa na msimu mzuri katika Serie A ndani ya kikosi cha Parma.

Kikosi cha Ivory Coast:

Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe), Ali Badra (Free State Stars), Tape Ira (FC San Pedro)

Mabeki: Serge Aurier (Tottenham), Wilfried Kanon (ADO The Hague), Wonlo Coulibaly (ASEC Mimosas), Ismaël Traoré (Angers), Mamadou Bagayoko (Red Star), Cheikh Comara (Wydad Casablanca), Souleyman Bamba (Rennes)

Viungo: Jean-Philippe Gbamin (Mainz), Geoffrey Serey Dié (Neuchâtel Xamax), Jean-Michael Seri (Fulham), Victorian Angban (Metz), Franck Kessié (Milan) , Ibrahim Sangaré (Toulouse)

Washambuliaji: Max-Alain Gradel (Toulouse), Nicolas Pépé (Lille), Wilfried Zaha (Crystal Palace), Jonathan Kodjia (Aston Villa), Roger Assalé (Young Boys Bern), Maxwel Cornet (Lyon), Wilfried Bony (hana klabu).