Zahera: Bahati yao tumewakosa!

Saturday January 19 2019

 

By Masoud Masasi.

 Kocha Mwinyi Zahera amesema katika mchezo wao dhidi ya Stand United walikosa bahati licha ya kucheza vizuri kuliko wapinzani wao.
Timu hiyo ya Shinyanga maarufu Chama la Wana imeifanyia mbaya yanga baada ya kuwafunga bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa.
Katika mchezo huo bao la ushindi la Stand United kwenye mchezo huo lilifungwa na Strains Jacob Masawe dakika ya 87.
Yanga ambao katika mchezo huo ndio ulikuwa wa kwanza kupoteza waliweza kukosa mabao ya wazi kupitia kwa Ibrahim Ajib na Heritier Makambo.
Ushindi huo wa Stand umeifanya kufikisha alama 25 huku Yanga wakibaki na pointi 53

Kocha Stand United, Athumani Bilali alisema japo wamepata ushindi lakini vijana wake hawakucheza kama alivyotaka haswa eneo la ushambuliaji kwani walikosa nafasi ambazo zingewapa ushindi.

Advertisement