Zanzibar yajaza viungo ikiivaa Sudan Chalenji

Muktasari:

Zanzibar imetwaa ubingwa wa mashindano ya Chalenji mara moja ambapo ilikuwa ni mwaka 1995

Kampala, Uganda. Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar kimeanza na wachezaji sita viungo wakati ikiivaa Sudan, mchana huu katika mechi ya mashindano ya Chaleni inayochezwa kwenye Uwanja wa KCCA jijini Kampala.

Kocha Hemed Morocco ameanzisha kundi kubwa la wachezaji ambao wanacheza katika nafasi hiyo akionekana kulenga kuwadhibiti zaidi wapinzani wao katikati.

Wachezaji hao ni Abdallah Kheri, Mudathir Yahya, Feisal Salum, Mohamed Issa 'Banka' na Awesu Awesu.

Wakati Abdulaziz Makame na Mudathir Yahya wakianza kama viungo wawili wa ulinzi, juu yao wapo watatu ambao ni Banka, Awesu na Feisal 'Fei Toto'

Abdallah Kheri yeye ameanza katika nafasi ya beki wa kati akicheza sambamba na Ali Ali.

Kikosi cha Zanzibar kinaundwa na wachezaji Suleiman Ahmed, Omar Ame, Haji Mwinyi, Ali Ali, Abdallah Kheri, Abdulaziz Makame, Mohamed Issah, Mudathir Yahya, Ibrahim Ilika, Feisal Salum na Awesu Awesu