Zidade ashusha presha Barca ikilala nyumbani

Barcelona, Hispania Real Madrid leo imekwepesha mzozo kwa njia bora baada ya kuinyuka Barcelona ugenini kwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza baina ya vigogo hao kufanyika bila ya mashabiki.
Ushndi huo umekuwa pigo la kwanza kwa Barca katika mbio za ubingwa.
Barca ilikuwa na nafasi ya kuipa Real kipigo cha tatu mfululizo na kumuongezea presha Zinedine Zidane.
Badala yake, ushindi wa Madrid umewafanya wawe juu ya wapinzani wao kwa tofauti ya pointi sita, wakiwa wamecheza mechi moja zaidi.
"Ni pointi tatu tu, lakini lazima tuzifurahie hasa baada ya mechi kusemwa kuhusu kikosi hiki," alisema Zidane.
Penati iliyopigwa na Sergio Ramos na bao lililofungwa mwishoni mwa Luka Modric liliimaliza Barcelona baada ya Federico Valverde na Ansu Fati kufunga mabao yao mapema katika mechi ambayo ilikwenda tofauti na wale waliokuwa wakihitaji ushahidi zaidi kwamba vigogo hao wanaporomoka.
"Mara kwa mara unakutwa na vipindi vibaya katika msimu na tunatumaini kuwa kipindi hiki kilidumu kwa wiki moja tu," alisema Ramos. "Kushinda mechi dhidi ya mpinzani wako wa muda mrefu kuliko wote ni kitu kinachoridhisha."
Barcelona inaweza kujiona imeshindwa kwa shida, hasa baada ya penati ya Ramos baada ya kufanyia uhakiki VAR na kuanguka kulikokuzwa na nahodha wa Madrid baada ya Clement Lenglet kumvuta jezi.
"Labda siku moja unaweza kuelezea VAR inafanyaje kazi hapa Hispania," alisema kocha Ronald Koeman. "Tulikuwa na mechi tano za ligi na VAR imeingilia tukio dhidi ya Barca."
Lakini ukiacha kipindi cha kwanza ambacho Lionel Messi alionyesha kutaka kuipa Barca ushindi kwa juhudi zake binafsi, Madrid ilitawala mchezo kwa vipindi virefu na kupata ushindi wakati ulipostahili.
Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza ya Classico kwa Ronald Koeman akiwa kocha wa Barcelona na baadhi ya presha ambazo Zidane angekabiliana nazo kama angeshindwa, sasa zitahamia kwa Mholanzi huyo, ambaye ameshashinda mechi tatu tu kati ya sita alizoiongoza timu hiyo hadi sasa.
Barcelona inakutana na Juventus Jumatano katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, bila ya Gerard Pique, ambaye anatumikia adhabu.