Zidane amkumbuka Bale Real Madrid

Monday August 12 2019

 

Rome, Italia. Mshambuliaji Gareth Bale amepewa dakika 30 kwa mara ya kwanza kucheza mechi ya ushindani ambayo Real Madrid ilinyukwa kwa penalti 5-4 dhidi ya AS Roma.

Baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, ilitumika mikwaju ya penalti na AS Roma ilishinda. Hii ni mara ya kwanza Bale kucheza mechi tangu dili lake la kwenda kucheza China kukwaa kisiki.

Kocha Zinedine Zidane alimjumuisha Bale katika kikosi cha wachezaji 20 kwenda Sweden kucheza mechi hiyo uamuzi ambao uliwashangaza wengi kutokana na uhasama waliokuwa nao wawili hao.

Bale aliwahi kukaririwa akisema hawazungumzi na Zidane kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipopewa kazi Real Madrid. Mara kadhaa kocha huyo amekuwa akikaririwa akisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, hayumo katika mpango wake.

Advertisement