Zitto anogesha mabao ya Okwi, Kagere

Saturday January 12 2019

 

MWANASIASA maarufu nchini Zitto Kabwe ameshindwa kuzuia mahaba yake baada ya Meddie Kagere kuiandikia Simba SC bao la tatu.

Simba SC  inaongoza uwanja wa taifa jijini Dar ea Salaam kwa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika.

Zitto ambaye amejichanganya na mashabiki huku akiwa na ulinzi mkali alitabasamu na kuanza kupiga makofi kufuatia Kagere kufunga bao hilo.

Baada ya mashabiki kumstukia kuwa waliyenaye karibu ni Zitto waliamsha shangwe la kumshangilia huku wakilitaja jina lake.

Zitto amekubali kusimama na kuufuatilia mchezo huo ambao Simba imeumiliki kwa kiasi kikubwa tangu kipindi cha kwanza ambacho walipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Advertisement