Mrembo Gigi avaana na aliyevamia jukwaa la Fashion Show

Wednesday October 2 2019

By AFP

Mrembo maarufu, Gigi Hadid amepambana na mwanamke mvamizi katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Chanel jijini Paris jana Jumanne baada ya mtu huyo kupanda jukwaani bila ya kuonekana na kutembea pamoja na warembo wengine wakati wa kumalizia onyesho.
Mwanamke huyo mchekeshaji wa Ufaransa alikimbia kutoka alipokaa na kuungana na ma-model wengine katika jukwaa ambalo lilipambwa kiufundi kuonyesha sehemu ya juu ya majengo ya jijini Paris kwenye ukumbi wa Grand Palais.
Huku walinzi wakiwa wameachwa solemba, Hadid alikabiliana na mvamizi huyo wakati akitaka kuwapita warembo hao.
Mvamnizi huyo, Marie Benoliel, mchekeshaji na ambaye katika Yuo Tube amejitambulisha kama Marie S'Infiltre (Marie Sneaks In), alikuwa amevaliarangi nyeupe na nyeusi kuanzia miguuni hadi kichwani na suti ya kitambaa cheusi yenye nakshi nyeupe na kofia.
Awali alivamia maonyesho ya mavazi ya ndani ya Etam jijini Paris akiwa amevalia nguo za ndani za rangi ya shaba na kufunika uso na kinywago cha kulalia.
Baada ya tukio hilo la Chanel alituma picha yake kwenye mtandao wa Instagram na kutangaza "Marie S'Infiltre strikes again (Marie S'Infiltre avamia tena)!"
Walinzi waligundua kuwa amevamia maonyesho ya mavazi wakati akiwa ameshamaliza alichokitaka.
"Sikuweza kujizuia kucheka kwa sababu walinzi hawakuweza kumuona," alisema mwandishi wa habari za mitindo ya mavazi wa New York, Elizabeth Paton, ambaye alikuwa amekaa viti vya safu ya mbele.
Wakati huo, Benoliel alikuwa akimalizia kutembea jukwaani akiwa ameweka mikono yake kiunoni kama supermodel.
dakika chache baadaye alipanga mstari pamoja na warembo wengine, lakini Hadid alikwenda kumzuia kabla ya kumuongoza kushuka jukwaani.
Kampuni ya Chanel iliiambia AFP kwamba mwanamke huyo aliwashangaza lakini "hii si mara ya kwanza kwake kufanya tukio hilo".
"Hatutakuza suala hilo," alisema msemaji wa Chanel.
"Tuingependa kwamba tukio hili lisingetokea."
Chanel ilisema baadaye Benoliel "alisindikizwa kutoka na walinzi."
Cardi B 'hakustushwa sana' -
Huku viti vya safu ya mbele vikiwa vimejaa watu maarufu kuanzia rapa wa Marekani, Cardi B hadi nyota wa pop, Jennie na muigizaji Mfaransa Isabelle Adjani, ulinzi ulikuwa mkali.
Cardi B alisema alipenda maonyesho hayo lakini alikiri baadaye alipoongea na gazeti la  Women's Wear Daily kwamba hakujali wakati mwanamke huyo alipochomoka na kwenda jukwaani.

Advertisement