Alichokifanya Cardi B kwa Offset hiki hapa

Tuesday July 23 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Marekani. Mkali wa miondoko ya Rap, Cardi B ameonyesha jinsi alivyofurahia kurudiana na mumewe Offset baada ya kuchora tattoo mguuni yenye jina la mwanaume huyo.

Wawili hao waliachana mwishoni mwa 2018 ambapo Cardi B baada ya mwanamke huyo kumlaumu Offset kwa kumsaliti na wanawake wengine.

Kwa mujibu wa tovuti ya Capital Xtra imeeleza kuwa rapa Offset aliiposti picha hiyo ya tattoo na kuadika, “Nachelea kusubiri kufika nyumbani.”

Katia ujumbe huo Offset ameweka  alama ya mchoro wa mdomo ukiwa umetoa ulimi nje kuonyesha kama ana uchu au anatamani kitu fulani.

Cardi B ni kama anajibu mapigo ya Offset ambaye aliwahi kuchora tattoo yenye jina la Cardi B shingoni pamoja na majina ya watoto wake wote wanne.

Advertisement