Baba Diamond apata mtoto mwingine

Tuesday April 9 2019

 

Abdul Juma, baba wa msanii Diamond Platnumz, amesema amepata mtoto mwingine wa hiyari anayeishi nchini Norway.

Akizungumza na Mwananchi, baba Diamond alisema mtoto huyo anayeitwa Patrick anataratajiwa kuja nchini siku za karibuni na kwamba alimpigia simu na kumueleza kuwa angependa kuja kumuona.

Alisema anajisikia faraja kwa watu kumtambua jambo ambalo anakiri limechangiwa na watoto wake kuwa maarufu.

“Unajua mtoto sio lazma awe uliyemzaa hata akijitokeza wa mtu mwingine na kutaka uwe baba yake ni jambo la heri kwani kuna wanaotamani iwe hivyo kwao lakini haijawatokea,” alisema.

Kuhusu mtoto wake wa Uingereza anayefahamika kwa jina la Zubeda, alisema bado wanawasiliana na huenda akija safari hii akaondoka naye kwa ajili ya kwenda kupata matibabu.

Zubeda hivi karibuni aliibua gumzo mitandaoni baada ya kueleza alifunga safari kuja nchini kuwapatanisha Diamond na baba yake huyo ambao wanaelezwa hawapo katika uhusiano mzuri. (Habari zote na Nasra Abdallah)

Advertisement