VIDEO: Baba Diamond ashiriki hafla ya mjukuu wake

Tuesday November 26 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Abdul Juma ambaye ni baba mzazi wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz ni kati ya watu walioshiriki hafla ya mjukuu wake iliyofanyika leo Jumanne Novemba 26, 2019.

Mtoto huyo wa Diamond na  Tanasha Donna alizaliwa Oktoba 2, 2019 jijini Dar es Salaam na kupewa jina la Naseeb Junior kwa kuwa alizaliwa siku na mwezi aliozaliwa Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul.

Baba yake Diamond aliwasili nyumbani kwa mwanaye saa 8:45 mchana muda mfupi baada ya kuanza hafla hiyo.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo ni  Queen Darleen, Rayavany, Romy Jones, Laizer, Moze Iyobo na Kulwa Kikumba maarufu  Dude.

Advertisement