Chidbenz kutunga wimbo kuhusu corona

Msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz akimweleza Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza (kulia) kuwa mapema wiki ijayo anatarajia kutoa video ya wimbo wake wa Beautiful na pia atatunga wimbo wa kuhusu Corona katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Muktasari:

Chidbenz amemuahidi Naibu waziri wa Sanaa, Juliana Shonza kuwa amebaduiika na hatarudi tena kutumia dawa za kulevya na huu ni mwezi wa tatu tangu aache.

Mwimbaji Rashid Abdallah maarufu Chidbenz amemuahidi Naibu Waziri Wizara ya Habari, Juliana Shonza kuwa atayunga wimbo kuhusu ugonjwa wa corona.
Chidbenz ametoa ahadi hiyo lieo, alipokuwa akizungumza na Naibu waziri huyo jijini Dodoma.
“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao ‘Beautiful’ ambao nimeuimba nikisifu uzuri wa mwanamke.
“Kufuatia janga la corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili wa kuelimisha,”amesema Chid benz.
Ameongeza kuwa “Ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara moja, nimekuwa naanguka nainuka narudi kwa mashabiki wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona ni wakati wa kuwafurahisha zaidi na sitawaangusha,”amesema Chdbenz.
Kwa upande wa Shonza amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa Chidbenz, baada ya kumuahidi kuwa amebadilika na ameachana na matumizi ya dawa za kulevya.
“Kwa sasa amesema anataka kuwaonyesha Watanzania amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya dawa za kulevya na hataki tena kurudi huko kwani ana zaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia.
“Kati ya wasanii wenye kukubalika  na mashabiki zao wewe Chidbenz  ni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kuanzia sasa unalijenga zaidi  jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika.
 “Wizara ipo pamoja  na wewe kukusaidia wakati wowote,”amesema Shonza alipokuwa akizungumza na msanii huyo.
 Shonza alimtaka msanii huyo kuwaonyesha  Watanzania kuwa anaweza na akipewa nafasi  ataonyesha juhudi ya utendaji kazi ikiwamo ubunifu.