Diamond aukubali muziki wa Ali Kiba

Thursday January 31 2019

 

By Nasra Abdallah na Helen hartley

Msanii Diamond ameonekana kushindwa kuvumilia utamu wa wimbo wa hasimu wake wa muziki Ali Kiba kwa kucheza wimbo wake .

Tukio hilo lilitokea leo katika viwanja vya Leaders ambapo Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda anatarajiwa kukutana na wasanii wa fani mbalimbali kwa ajili ya kuzungumza nao.

Wimbo huo sio mwingine bali ni ule wa 'Kadogo' ambao aliuachia mwishoni mwa mwaka Jana.

Timu ya MCL Digital iliyopo maeneo ya viwanja hivyo ilimshuhudia Diamond akiwa anatikisa kichwa kuonyesha kwamba kaukubali wimbo huo.

Hata hivyo baada ya wimbo huo kuisha DJ aliunganisha wimbo wa Diamond aliouimba na Harmonize wa 'Kwangaru'.

 

Advertisement