Diamond avunja rekodi yake

Wednesday June 26 2019

 

By Muyonga Jumanne, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa muziki  nchini Tanzania, Diamond Platnumz ni nooomaaa! Ndiyo unavyoweza sema kwa sasa baada ya kuanza kuvunja rekodi zake mwenyewe kwenye mtandao wa Youtube kupitia nyimbo zake mpya.

Wimbo mpya wa ‘Kanyaga’ aliyouachia video Juni 25, 2019 umefikisha watazamaji milioni 1 ndani ya saa 13, ni rekodi mpya kwake na muziki wa Bongo Flava akivunja za nyimbo zake mbili.

Mosi kavunja rekodi ya wimbo wa ‘Hallelujah’ aliowashirikisha kundi la Morgan Heritage kutoka nchini Jamaica ilifikisha watazamaji milioni 1 ndani ya saa 15.

Wimbo wa ‘Inama’ aliomshirikisha Fally Ipupa kutoka nchini DRC kuwekwa Youtube Juni 9,2019 kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali umefikisha watazamaji milioni 1 ndani ya masaa 16.

Advertisement