Duka la Nipsey Hussle lafungwa rasmi

Saturday June 1 2019

 

Duka la The Marathon lililokuwa likimilikiwa na rapa, Nipsey Hussle limefungwa rasmi. Taarifa ya familia yake imeeleza.

Nje ya duka hilo, Machi 30, rapa huyo mwenye asili ya Afrika aliuawa baada ya kushambuliwa kwa risasi kadhaa zilizompata kichwani na tumboni.

Taarifa ya familia imesema inalifunga duka hilo kwa sasa mpaka baadaye itakapofanya uamuzi mwingine ikisisitiza kuwa biashara itaendelea kwa njia ya mtandao. “Kwa wateja wetu ambao wameweka oda, tutawahudumia na pia mkumbuke biashara itakabaki mtandaoni kwa sasa mpaka familia itakapofanya maamuzi mengine.”

Advertisement