Hamisa Mobetto aupamba wimbo Dodo wa Ali Kiba

Muktasari:

Amerudi tena. Ndivyo ninavyoweza kusema  baada ya msanii Ali Kiba kutoa wimbo uitwao Dodo  katika mtandao wa Youtube leo asubuhi Jumatano Aprili 8, 2020.
 

Dar es Salaam. Amerudi tena. Ndivyo ninavyoweza kusema  baada ya msanii Ali Kiba kutoa wimbo uitwao Dodo  katika mtandao wa Youtube leo asubuhi Jumatano Aprili 8, 2020.

 

Hamisa Mobetto ndio aliyepamba video hiyo jambo lililoanza kuibua mjadala mtandaoni kutokana na kuwa mwanamitindo huo ni mzazi mwenzake msanii Diamond Platnumz ambaye ni mpinzani wa Ali Kiba katika tasnia ya muziki nchini Tanzania.

 

Katika video ya wimbo huo, Kiba anaonekana amevaa kama mfalme na Mobetto amevaa kama malkia na maeneo mengine kama bibi harusi.

 

Kiba kamshirikisha Mobetto katika wimbo huo ikiwa ni siku kadhaa baada ya mama huyo wa watoto wawili kuelezwa kuwa amerudiana na mzazi mwenzake Diamond.

Wimbo huo tangu uachiwe ndani ya saa saba ulikuwa umetizamwa na watu zaidi ya 50,000 katika mtandao wa Youtube, huku watu zaidi ya 10,000 wakitoa maoni yao yanayoonyesha kuikubali kazi hiyo kutoka Kings Music.

Miongoni mwa waliotoa maoni ni david curtis  aliyeandika “Dah! Hii nyimbo imetulia sana sana. 1-Beat 100% 2-uandishi 100% 3-wahusika 100 %”.

Ali Kiba mara ya mwisho kutoa wimbo ilikuwa Novemba 8,2019 uitwao ‘Mshumaa’.