Juma Nature: Kuvunjika makundi kunakuza muziki

Tuesday October 15 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi

Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Juma Nature amesema kuna baadhi ya faida zinazotokana na kuvunjika kwa makundi ya muziki, tofauti na mtizamo wa wengi.

Juma Nature ni kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK wanaume Family lililojizolea umaarufu kabla ya kuvunjika mwaka 2006 huku likiwa limesheheni wasanii kama Yp, Y Dash, Chege, KR Mula, Luten Kalama, Mzimu, Malipo, Nature,  Dolo na Stico.

Baada ya kuvunjika kwake, Nature na baadhi ya wasanii waliokuwepo TMK wanaume akiwemo Dolo, Luteni Kalama, Mzimu, Malipo na D Chief walienda kuunda kundi walilolipa jina la Wanaume Halisi.

Akizungumzia leo Jumanne Oktoba 15, 2019 na Mwananchi kuhusu vitendo vya kuvunjika kwa makundi kama haoni inaleta shida kwenye muziki, msanii huyo amesema kwake anaona ina faida ikiwemo kuendelea kukuza muziki.

Amefafanua kila msanii anapotawanyika anaongeza ushindani kwa sababu anaua walikuwa wanafanya nini walipokuwa kwenye kundi.

 “Kuvunjika kwa makundi hakujaanza jana wala leo hata huko Marekani ambako wameanza muziki siku nyingi tulishuhudia makundi mengi kuvunjika, lakini ndio kwanza muziki wao umezidi kukua siku hadi siku.

Advertisement

“Hata hapa kwetu vilevile tuna mifano hai kwani baadhi ya waliokuwa kwenye makundi na kwenda kuanza kazi kivyao walileta ushindani katika soko la muziki na ndio maana sasa hivi Bongofleva inajulikana maeneo mbalimbali barani Afrika.

Amesema  kuna wakati akili inachoka mkikaa pamoja muda mrefu, hivyo mkitengana kila mmoja atatoka nje ya boksi.

Advertisement