Kitambi cha Chioma gumzo Nigeria

Monday June 3 2019

 

Chioma maarufu  Chef Chi  ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Davido, huenda akampatia  mtoto wa tatu mwimbaji huyo wa Skelewu.
Blogu maarufu inayofuatilia maisha ya wasanii nchini Nigeria, Instablogia  imeweka kipande cha video ya  Chioma na Davido kikimuonyesha kuwa na tumbo kubwa huku mashabiki wakidai haliwezi kuwa la kawaida bali ujauzito.
Pamoja na kutabiri na kufurahia, mashabiki wa walimwandama Davido kwa maswali wakimuuliza atamuoa lini msichana huyo mwenye umri wa miaka 24.
Baada ya kuweka mahusiano yao wazi mwaka 2017, wawili hao wamepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii na kushika vichwa vya habari barani Afrika na kwingineko duniani.

Advertisement