Lady Jay Dee hatupi nguo

Saturday November 10 2018Judith Wambura, Lady Jay Dee, Komando, Anaconda

Judith Wambura, Lady Jay Dee, Komando, Anaconda 

Muite Judith Wambura, Lady Jay Dee, Komando, Anaconda na majina mengine mengi yanayoashiria ukomavu katika sanaa ya muziki Afrika Mashariki.

Pamoja na kuwa katika ramani ya muziki kwa zaidi ya miaka 15, Lady Jay Dee anajitofautisha na wanamuziki wa kike kitabia na mavazi.

Wasanii wengi wana hulka ya kutorudia mavazi hasa yale wanazopita nazo katika zulia jekundu wakati hafla maalum.

Lady Jay Dee ambaye hivi karibuni alifanya tamasha lenye mafanikio la Vocal Night, anasema pamoja na ustaa wake huwa anapata wakati mgumu kuacha kuirudia mara kwa mara nguo anayipenda, hata zile anazopita nazo kwenye zulia jekundu.

Anasema hadi aamue kuvaa nguo fulani, ina maana ilimvutia na kila wakati angependa kuiona ikikaa mwilini.

“Jamani mtambue na sisi tuna maisha yetu nje ya usanii,” anasema Jay Dee ambaye alichomoza kimuziki na kibao cha “Machozi” kilichomfanya apachikwe jina la Binti Machozi.

“Kwa nini niuze nguo niliyoinunua kwa fedha zangu, kisa tu sitaki kurudia kuivaa? Hapana, kuliko kufanya hivyo bora niiweke ndani.

“Pia huwa inauma nguo umeivaa mara moja halafu uiache kuivaa kwa kuwa unaweza kupata mtoko wa siku nyingine ukaivaa vizuri tu bila shida.”

Advertisement