Lulu na Hamisa Mobeto kumbe fresh tu

Sunday February 24 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini Tanzania  Elizabeth Michael 'Lulu' jana usiku Jumamosi Februari 23, 2019 katika utoaji wa tuzo za  Filamu Zetu International Festival Film (SZIFF) mwaka 2019  alimuita kwa mbwembwe jukwaani mwanamitindo, Hamisa Mobeto.

Lulu aliyekuwa msherekeshaji wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam alimuita Mobeto kwa staili ya aina yake na kuibua shangwe kwa watu waliokuwa ukumbini.

“Ninamleta kwenu model,  mrembo, mama wa watoto wawili jukwaani na si mwingine ni Hamisa Mobeto,” amesema Lulu.

Baada ya kupanda jukwaani Mobeto alimkabidhi tuzo mmoja wa washindi na kurejea alikokuwa amekaa.

Advertisement