Mama mzazi wa Isha Mashauzi afariki dunia

Wednesday May 29 2019

 

By Rhobi Chacha, Mwananchi

Mmiliki na mwanamuziki  wa kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani maarufu ‘Isha Mashauzi’ amepata pigo baada ya kumpoteza mama yake mzazi, Rukia Juma aliyefariki dunia leo Mei 29, mwaka 2019.
Bi Rukia Jumaa ambaye pia alikuwa mwimbaji wa taarabu katika bendi ya Mashauzi Classsic  na TOT Taarab, amefariki jioni hii njiani akiwa anapelekwa Hospitali ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa Abdul Said aliyejitambulisha kuwa ndugu wa karibu na familia hiyo, amsema Bi Rukia alikuwa anaumwa lakini alizidiwa na kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hopitali ya Taifa Muhimbili.

Said amesema kwa sasa Msiba upo nyumbani kwa Isha Mashauzi Kinondoni Hananasifu hadi itakapofika saa tatu msiba utapelekwa Mbezi kwa Msuguri alipokiwa akiishi Bi Rukia

Hili ni pigo kwa mwanamuziki Isha ambaye miaka minne iliyopita alimpoteza baba yake mzazi, Ramadhani Makongo.

Advertisement