Msiba wa mtoto Patrick watua Mwananyamala kwa baba mzazi

Wednesday July 4 2018

 

By Rhobi Chacha

 Wakati watu wanasubiri kuupokea mwili wa mtoto Patrick aliyefariki  jana Jumanne usiku wakiwa Nairobi, Kenya akipatiwa matibabu.

Dada wa Muna, Eve amefunguka na kusema msiba uko kwa baba wa mtoto, Peter anayeishi Mwananyala kwa Mwakibile jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital, Eve amesema, wameamua kuweka msiba Mwananyamala ,kwa sababu ndiko nyumbani kwa baba yake Patrick.

“Msiba hauko huko Mbezi jamani, Patrick ana baba yake yuko hai anaitwa Peter, hivyo tuko hapa Mwananyamala maarufu kwa Mwakibile na hapa tunapanga jinsi ya kuurudisha mwili Tanzania kwa ajili ya maziko, ambayo tutawatajia siku ya kuzika.”

Hata hivyo Eve aliomba watu waachane na habari za mitandaoni, kwani asilimia kubwa zinapotosha. Alisema wakitaka ukweli waende msibani kwa ajili ya kupata habari kamili.

Mbali na hiyo Eve alisema, Patrick ameumwa kwa wiki mbili, kutokana na kusumbuliwa  uvimbe kichwani.

“Nimerudi jana tu, huku nyuma napata habari Patrick amefariki, imenuima sana, tulimpeleka Nairobi kwa ajili ya matibabu ya kichwa, kilikuwa kinamuuma kila wakati, ambacho kilisababishwa na uvimbe kichwani, ila ndio hivyo Mungu amempenda zaidi.”

Aidha alikana kuwa habari zinazodaiwa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa Patrick ni mtoto wa mtangazaji wa Clouds, Caston.

“Kama nilivyokwambia mwanzo, watu wasipende kuongea vitu ambavyo hawavijui, ukweli ni kwamba Caston sio baba wa Patrick kama inavyodaiwa, hivyo watu waachane na hizo habari za mitandaoni jamani,”alisema Eve.

Advertisement