Meek Mill kufungua madai ya kubaguliwa kwa rangi yake

Saturday June 1 2019

 

Sasa ni zamu ya Rapa Meek Mill kusimama mahakamani akiwa kama mshtaki kwa kile alichodai kubaguliwa na viongozi wa hoteli ya Cosmopolitan iliyopo Las Vega, nchini Marekani.

Mwanasheria wa Mill, Joe Tacopina amesema mteja wake alibaguliwa kwa misingi ya rangi yake na kwamba sio wa kwanza kwani wengine wenye asili ya Afrika, Yo Gotti na Blocboy JB waliwahi kuishtaki kwa matukio kama hayo.

Tacopina amejiapiza kwamba atakachofanya atakahikikisha hoteli hiyo inapoteza kila kitu ili iwe fundisho kwa wengine wanaobagua Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Inaelezwa kuwa Mill alifika hotelini hapo kuonana na rafiki yake, DJ Mustard lakini alipozuiliwa kumuona aliwaambia wamuache akanunue chakula.

Walinzi walimueleza kuwa asingeweza kupata huduma hiyo kwa wakati ule kitu ambacho Tacopina anasema si cha kweli kwa kuwa hoteli hiyo huwa inatoa huduma ya chakula kwa saa 24. Baada ya tukio hilo, Tacopina aliuandikia uongozi wa hoteli barua akitaka wameuombe radhi.

Advertisement