Mr Beneficial adai, macho ya watu yanamtafsiri ndivyo sivyo

Monday July 1 2019

 

By Nasra Abadallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa vichekesho nchini Tanzania, Brian Mrikaria maarufu ‘Mr Beneficial’ amesema nguo anazozivaa wakati wa kuigiza sio kubwa.

Katika mahojiano maalum na Mwananchi, leo Jumatatu Julai mosi, 2019 amesema kwake viatu na nguo vyote anavyovaa ni saizi yake.

Huku akieleza kuwa kwa watu wanaomuona kwamba kavaa viatu ‘oversize’ wajue kwamba vinambana.

Wakati kwa wale wanaoona kavaa nguo kubwa kuzidi  mwili wake, wao macho yao ndio makubwa na sio nguo zake.

Mr Beneficial ni kati ya wachekeshaji walioteka mitandao ya kijamii kwa sasa kutokana na staili yake ya uigizaji huku kubwa ikiwa kuongea lafudhi ya watu wa pande za Arusha.

Kampuni Timamu, anayofanya nayo kazi kwa sasa, ndio iliyomrudisha kwenye soko la sanaa ya uigizaji,  marehemu King Majuto na kumpa umaarufu marehemu Sharomilionea.

Advertisement

Wengine waliopitia katika mikono ya kampuni hiyo ni pamoja na ‘Mkali wao’ na Ebitoke ambao kwa sasa wameamua kufanya kazi kivyao.

Kujua mengi zaidi kuhusu Mr Beneficial, usikose gazeti lako la Mwananchi la Jumamosi Julai 6, 2019

Advertisement