Msanii Munalove awavalisha watoto wa Zari

Thursday February 20 2020

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Munalove ambaye ni Mjasiriamali na msanii, hivi karibuni amelamba dume baada ya kujikuta akiingia kwenye makubaliano ya kibiashara na  Zarina Hassan maarufu Zari.

Muna ambaye jina lake halisi ni Rose Alphonce, amefichua siri hiyo katika mahojiano maalumu na Mwananchi ambalo lilimtafuta kutaka kupata ufafanuzi wake baada ya kuona amewaweka watoto wa Zari, Tiffah na Nillan katika ukurasa wake wa Instagram na kumshukuru staa huyo kutoka nchini Uganda.

“Mmependeza, nashukuru Zari kwa kuniamini,” ameandika Munalove.

Muna ameliambia Mwananchi kuwa; “Nimeingia makubaliano na Zari ya kuwatumia watoto wake nguo kila mwisho wa mwezi na yeye hunitumia fedha kwa njia ya benki.

 

Amelipataje dili hilo?

Advertisement

“Mwaka jana nikiwa nchini China Zari alinipigia simu akanipa oda ya nguo za Nillan kwa ajili ya kuvaa siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

“Nikamtumia nilizonazo achague kisha akanitumia hela nami nikamtumia mzigo na ndio kuanzia hapo akanipa oda kila mwisho wa mwezi nimtumie nguo,” amesema mjasiriamali huyo.

Amesema anajisikia furaha na kama ataendelea kupata wateja wa aina ya Zari, kwake itakuwa furaha zaidi.

“Kwa kweli nashukuru sana na siku zote Mungu ni mwaminifu hawezi kukuacha," amesema Munalove.

 

Advertisement