Mwanasheria wa Jay-Z abeba kesi ya rapa 21 Savage

Muktasari:

  • Nyota huyo wa muziki wa hip-hop anadaiwa kuwa si raia wa Marekani, lakini wanasheria wake wanasema kwa kuwa tayari ana watoto watatu ambao wana uraia, ana sifa za kutotimuliwa.

Mwanasheria ambaye amekuwa akimtetea rapa tajiri, Jay-Z, anamtetea mwanamuziki chipukizi katika miondoko ya rap, 21 Savage, ambaye anakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa na Idara ya Uhamia ya Marekani, akisema kijana huyo hana utaifa wowote.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 26 na ambaye nyimbo zake zinatamba kwenye chati za muziki--jina lake halisi ni Sha Yaa Bin Abraham-Joseph -- alikamatwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji mwishoni mwa wiki katika jiji lililo kusini mwa Atlanta waskidai viza yake ya kuishi Marekani iliisha mwaka 2006.
Alex Spiro, mwanasheria wa jijini New York ambaye amewahi kuwakilisha wasanii kadhaa maarufu, amechukua kesi hiyo kwa maombi ya Jay-Z.
Mwanasheria hiyo aliiambia AFP kwamba 21 Savage, ambaye ametajwa kuwania tuzo za Grammy, amehifadhiwa kwenye kituo kilicho karibu na Atlanta na ametaka aachiwe kwa dhamana.
Spiro alisema maombi ya viza yaliyowasilishwa na 21 Savage yamezuiwa lakini atahakikisha chipukizi huyo anapata hadhi ya uhamiaji.
"Kukamatwa kwa 21 Savage ni dhihaka kabisa, maombi yake ya U Viza hayajashughulikiwa kwa miaka minne," Jay-Z aliandika katikia ukurasa wake wa Facebook.
U Visa hutolewa kwa watu ambao ni waathirika wa uhalifu ambao wamewahi kukumbana na kunyanyaswa kiakili au kimwili. Awali timu yake ilisema iloiwasilisha maombi hayo kwa sababu ya kumbukumbu aliyonayo kwa kuwa alishuhudia mauaji ya kutisha ya risasi mwaka 2013.
Timu ya wanasheria wake ilisema awali kuwa rapa huyo aliwasili Marekani akiwa na umri wa miaka saba na akaishi kwa miaka 20 mfululizo, isipokuwa alipokwenda kwa muda mfupi nchini Uingereza mwaka 2005.
Kwa mrefu 21 Savage amekuwa akichukuliwa kuwa ni msanii kutoka Atlanta ambao ni kama mji mkuu wa muziki wa hip-hop.
Nyota huyo chipukizi ana watoto watatu ambao ni raia wa Marekani, kitu ambacho wanasheria wake wanasema kinamfanya awe hastahili kutimuliwa Marekani.
"Zaidi ya kuwa mwanamuziki mwenye mafanikio, 21 anastahili kurudi kuungana na familia yake mara moja," alisema Jay-Z. AFP