Ndoa ya Nick Minaj, Petty ndani ya siku 80

Wednesday August 14 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Los Angeles, Marekani. Imethibitika kuwa rapa Nick Minaj na mpenzi wake Kenneth Petty wamepewa siku 80 za kukamilisha mipango ya ndoa yao.

Wawili hao Julai 29, 2019 walionekana pamoja mahakamani wakiwa wamepanga foleni ya kuchukua leseni ya ndoa jambo lilizaa uvumi kuwa wanataka kufunga ndoa.

Tovuti ya TMZ imetaarifu kuwa kupitia  Queen Radio inayomilikiwa na rapa Nicki Minaj, rapa huyo  aliweka wazi kuwa wamepata leseni kwa mara ya pili inayowataka kufunga ndoa ndani ya siku 80.

Amesema awali waliwahi kupata leseni ya ndoa, lakini kutokana na kubanwa na ratiba  ya shughuli zao leseni ilikwisha muda kabla ya kufunga ndoa.

Nicki Minaj na Kenneth  walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2018. Minaj ameeleza kuwa watafunga ndoa na kufanya hafla ndogo, kabla ya kutayarisha sherehe kubwa siku za usoni.

Advertisement