Rap yatingisha tuzo za Grammy

Cardi B a\kitgoa hotuba ya shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya Albamu Bora ya Rap usiku wa kuamkia leo. Kushoto kwake ni mumewe Offset. AFP

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza kwa wasanii wa muziki wa rap kutwaa tuzo kubwa kama "Rekodi ya Mwaka" na "Wimbo wa Mwaka" katika tamasha la muziki wa Grammy linalofanyika kila mwaka nchini Marekani. Rapa wa kike, Cardi B pia amekuwa mwanamke wa kwanza kutwaa tuzo ya Albamu ya Bora ya Rap.

Muziki wa rap umeweka historia katika tuzo maarufu duniani za Grammy baada ya wasanii wake kutamba katika siku ambayo wanawake pia waliandika historia mpya.
Cardi B amekuwa msanii wa kwanza wa kike kutwaa tuzo ya Albamu Bora ya Rap wakati Childish Gambino alishinda tuzo nyingine mbili kubwa za Rekodi ya Mwaka na Wimbo wa Mwaka.
Tuzo ya Rekodi ya Mwaka hutambua wasanii, watayarishaji na wahandisi waliochangia katika kurekodi wimbo ulioshinda, wakati Wimbo wa Mwaka hushughulika na utunzi wa wimbo na hivyo tuzop huenda kwa aliyeuandika.
Kwa mwaka wa pili mfululizo, wasanii weusi wa miondoko ya hip-hop walitawala tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya 61 tangu kuanzishwa. Tamasha hilo lilifanyika ukumbi wa Stapple Center jijini Los Angeles, California nchini Marekani usiku wa kuamkia leo.
Lakini tofauti na miaka iliyopita, safari hii wasanii hao weusi walishinda tuzo kadhaa kubwa -- labda ikiwa ni ishara kuwa taasisi inayoandaa tuzo hizo ya Recording Academy inaanza taratibu kuzoea utamaduni wa muziki wa pop.
Ushindi wa Cardi B uliotokana na albamu yake ya "Invasion of Privacy (kuingilia faragha)" ulikuwa ni kutambua mafanikio ya msanii huyo ambaye sasa anatawala chati za muziki wa hip-hop unaotawaliwa na wanaume.
Malkia huyo wa rap mwenye umri wa miaka 26 aliwashinda Mac Miller na Travis Scott alipotwaa tuzo hiyo ya kwanza kwake ya Grammy katika maisha yake ya muziki, akiwa ameanza kuchomoza na kibao kilichotamba cha "Bodak Yellow".
Akionekana dhahiri kutetemeka, na akiwa ndio kwanza ametoka kutumbuiza kibao chake cha "Money kwenye hafla hiyo,", Cardi B alitoa hotuba ya kushukuru iliyokuwa na hisia akiwa pamoja na mumewe, Offset wa kundi la wasanii watatu wa rap la Migos.
"Neva ni mbaya sana. Labda nianze kuvuta bangi," alisema msichana huyo huku akicheza, kabla ya kumgeukia Offset na kusema: "Wewe mume, asante."
Mvuto wa Cardi B unaonekana kwenye albamu nzima, ambayo inaelezea jinsi alivyopanda chati katika muziki.
Nyota huyo mzaliwa wa Belcalis Almanzar alitoa nyimbo kwa ajili ya filamu wakati wa majira ya joto mwaka 2018 kutokana na kibao chake cha "I Like It," ambacho kinaenzi asili yake ya Amerika Kusini kwa kuweka viwango vya boogaloo vya miaka ya sitini.
Katika moja ya albamu zilizokuwa na mafanikio makubwa mwaka 2018, taasisi inayounganisha wasanii wanaorekodi muziki ya Amerika (Recording Industry Association of America) ilipitisha nyimbo zote zilizo katika albamu ya "Invasion of Privacy" kuwa zilifikia kiwango cha "dhahabu" au juu zaidi.
Hiyo inamfanya Cardi B kuwa msanii wa kwanza wa kike wa muziki wa rap kufikia mafanikio makubwa katika mauzo ya albamu hiyo.

Cardi B akiwasili kwenye tamasha la kutuza wanamuziki nchini Marekani la Grammy usiku wa kuamkia leo. AFP



Gambino atamba
Childish Gambino alitwaa tuzo mbili za Rekodi ya Mwaka na Wimbo wa Mwaka, ikiwa ni mara ya kwanza kwa msanii wa rap kupata mafanikio hayo.
Gambino alikuwa mmoja wa wanamuziki waliong'ara usiku wa jana, akiwa ameshinda tuzo nne, nyingine zikiwa ni ya kurap vizuri (Best Rap/Sung Performance) na Video Bora ya Muziki kutokana na kibao chake cha "This Is America."
Lakini hakutokea kwenye tamasha hilo kufurahia mafanikio hayo.
Wenzake waliwaambia waandishi wa habari kuwa hawajui sababu za kutohudhuria, lakini aliripotiwa kuwa alikataa mwaliko wa kutumbuiza katika tamasha hilo.
"Nadhani kama ukisiliza redio au kama ukiangalia utamaduni wetu, kama ukiangalia nyimbo zilizopakuliwa mara nyingi, unaona kitu ambacho kinafurahisha watu," alisema Ludwig Goransson, ambaye aliandika wimbo wa "Gambino".
"Ni suala la muda tu kwamba vitu kama hivi vinatokea katika tuzo za Grammy," aliwaambia waandishi wa habari baada ya hafla hiyo. "Wanaanza kupata hisia sawasawa na watu wengine."
Wimbo huo wa injili umejaa maoni ya kijamii yanayoenda sambamba na rhythm ya kasi, mapambio ya kanisani na midundo ya Afro na gitaa zito la besi.

Anderson .Paak, mshindi wa tuzo ya Best Rap Performance (inayoangalia ustadi katika kurap--kasi na pumzi) kutokana na kibao chake cha "Bubblin" akiwa na tuzo zake pamoja na Soul Rasheed usiku wa kuamkia leo.



Drake alishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Rap kutokana na kibao chake cha "God's Plan," ushindi wake pekee licha ya kutajwa kuwania tuzo saba.
Rapa huyo wa Canada -- ambaye alikuwa na mzozo na Recording Academy miaka iliyopita -- alijitokeza kupokea tuzo yake licha ya kuenea uvumi kuwa asingetokea.
Kendrick Lamar, ambaye aliongoza kwa kutajwa kuwania tuzo nane, alipata ushindi wake wa kwanza usiku wa jana kutokana na kibao chake cha "King's Dead," ambacho ameimba pamoja na Jay Rock, Future na James Blake. AFP