Teknolojia: Tumia USB Condom kuikinga simu yako unapo-charge

Taarifa katika simu yako ya mkononi zinaweza kudukuliwa kwa urahisi pale unapochaji simu katika maeneo yanayo-tumiwa na watu wengi kama vile uwanja wa ndege, migahawa na hata usafiri wa umma.

Wengi wetu tunapenda kuzitumia kuchaji simu, hata unapoikuta simu ya mwenzako unaweza kuiondoa na kuweka ya kwako bila kujua unajiweka katika hatari ya kusambaza taarifa zako.Utafiti uliofanywa na kampuni ya Kaspersky Labs ya Uingereza umegundua kuwa upo uwezekano wa kuingiziwa app za hatari katika simu hiyo bila mhusika kufahamu na kisha taarifa zako kuduku-liwa kwa kipindi chote atakachoitumia simu yake.Pia, utafiti huo umegundua app hiyo inaweza kuingizwa kwa muda usiozidi dakika tatu tu iwapo mhusika atachaji kwa waya wa USB.

Hata hivyo, unaweza kuikinga simu yako kwa kuweka kifaa kiitwacho USB Condom ambacho huchomekwa katika sehemu ya chini ya simu.Kifaa hiki huzuia kuingiza virusi au kudukuliwa taarifa zako zikiwamo picha na video zilizopo katika simu yako.