Video ya Harmonize, Rayvanny ni mshikemshike mtandaoni

Tuesday December 3 2019

 

By Exaud Mtei, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Video ya nani kali. Ndio mjadala ulioshika kasi katika mitandao ya kijamii mashabiki wakihoji video ipi kali kati ya wimbo Kushoto Kulia wa msanii Harmonize na Tetema Remix wa Rayvanny.

Jana Jumatatu Desemba 2, 2019 Harmonize aliachia video hiyo katika mtandao wa Youtube na siku hiyohiyo Rayvanny naye alitoa video ya Tetema Remix  akimshirikisha Diamond Platnumz, Pantoranking na Zlatan.

Hadi leo Jumanne Desemba 3, 2019 saa 9:00 alasiri wimbo Kushoto Kulia ulikuwa umetazama mara 446, 313 na Tetema mara 60,876.

Kushoto Kulia umeingia katika orodha ya video zinazotazamwa zaidi katika mtandao huo ukiwa nafasi ya nne.

Wafuatiliaji wa muziki wa kizazi kipya nchini wamekuwa na maoni tofauti kuhusu video hizo.

Mmoja wa wachangiaji,  the_kid_rich_48 amesema, “nataka kuona nani atakuwa number one on trending  YouTube maana Harmonize katoa kushoto kulia, Diamond Platnumz kaachia behind the scenes ya babalao, rayvanny kaachia remix tetema huu mwaka unaisha pazuri.”

Advertisement

Sivikson Lubogo4, “naona upande wa pili wameachia remix ya tetema ili watudhoofishe but hawatoweza, mambo ni..”

Kwa upande wake Nguya MtwarTz7 amesema, “ndugu zetu washaanza fitina, konde boi jeshi unawindwa pambana sana tupo nyuma yako.”

H matta Kimbunga amesema, “kwa hiyo  hamtaki mmakonde akakae no1 on trending au maana sijawaelewa kabisa dhamila yenu.”

Advertisement