Werrason kupiga kolabo na Diamond, kuwasha moto kesho Dar

Saturday July 7 2018Msanii Noel Ngiama 'Werrason'.

Msanii Noel Ngiama 'Werrason'. 

By Saddam Sadick

Mwanza. Msanii Noel Ngiama 'Werrason'  ametua nchini na anatarajia kufanya kolabo na Diamond Platnumz  ikiwa ni mkakati wake wa kuwainua wasanii  na kudumisha muziki wa Afrika.

Werrason alisema  azma yake kubwa ni kuinua wasanii na tayari amefanya kolabo na Bella na anayefuata ni Diamond,  huku akisisitiza kwamba atashirikiana pia na wasanii wengine.

Werrason anatarajia kutoa burudani nzito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, shoo itakayofanyika katika Ukumbi wa Rock City

Akizungumza jijini hapa leo Jumamosi, Werrason alisema ameamua kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na mikoa jirani ikiwa ni mkakati wake wa kudumisha muziki wa Afrika.

Amesema kuwa baada ya shoo leo jijini Mwanz\a, moto utawaka jijini Dar es Salaam kesho Jumapili katika viwanja vya Live Park Mwenge ili kuhakikisha anakata kiu ya Watanzania katika kazi yake ya muziki.

"Leo nitakuwa pale Rock City,kesho Dar es Salaam na hii ni kwa sababu nataka kudumisha muziki wa Afrika" amesema Werrason.

Msanii huyo maarufu ameongeza kuwa lengo la ujio wake hapa nchini ni kutaka kuinua Wasanii katika anga za muziki na kwamba baada ya kufanya kolabo na Christian Bella sasa ni zamu ya Diamond.

"Nataka kuinua Wasanii wa Tanzania na tayari nimeshafanya 'feature' na Bella na sasa nasubiri Diamond arudi nchini ili tufanye wote,lakini pia si hao tu bali wapo wengine " amesema Msanii huyo.

Advertisement