#WC2018: Historia nyingine ya Harry Kane ya kusisimua

Wednesday July 4 2018

 

By Evagrey vitalis

Nahodha wa timu ya Taifa ya England anayecheza klabu ya Tottenham Hotspurs ya England, Harry Kane ana historia ya kuvutia katika maisha yake.

Miaka 13 iliyopita Kane ambaye kwa sasa ni nahodha wa England, alikuwa na ndoto ya kukutana na kupiga picha na staa wa England wa wakati huo David Beckham lengo ambalo alilitimiza.

Jana Jumanne usiku, Harry Kane aliweka historia ya kuwa nahodha wa kwanza kuwahi kuiongoza England, kwenye robo fainali baada ya kuweka wavuni bao kwa mikwaju ya penati na kushinda dhidi ya Colombia.

 Hiyo ni baada ya dakika 120 kumalizika matokeo yakiwa 1-1, ndio England ikapata ushindi wa penati 4-3.

Katika picha inayosambaa mtandaoni ya story ya kuvutia ya Harry Kane akiwa na David Beckham aliipiga picha hiyo ikiwa ni miaka 13 iliyopita akiwa yeye, mchezaji mwenzake wa kike na Beckham lakini leo Kane amekuwa staa na yule mchezaji wa kike waliopiga picha na Beckham miaka hiyo amekuwa mkewe.