Joshua kuzipiga Wembley Stadium

Monday July 9 2018

 

London, England. Bondia bingwa wa Dunia uzito wa juu duniani, Anthony Joshua wa Uingereza, amesaini mikataba miwili ya kuzipiga kwenye uwanja wa Wembley, nchini Wales.

Joshua mwenye miaka 28, ambaye sasa anasimamiwa na Kampuni ya uporomota ya Matchroom Boxing, pambano lake la kwanza litafanyika Septemba 22 mwaka huu wakati la pili litakua Aprili 13 mwakani.

Bingwa huyo wa Dunia anayetambuliwa na WBA, IBF na WBO, alimstaafisha ngumi mbabe wa Ukraine, Wladimir Klitschko, baada ya kumchapa kwenye pambano lililofanyika Wembley Aprili, 2017.

Joshua aliyeshinda mapambano yake mawili yaliyofuata dhidi ya Carlos Takam na Joseph Parker kwenye uwanja wa Principality nchini Wales, ameelezea kufurahia kucheza tena nchini Uingereza.

"Nimezaliwa na kukulia London, Uingereza ni nchi yangu ya damu kwa hiyo ninapopata nafasi ya kucheza katika ardhi hii ninakua na furaha na naahidi kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wangu,” alisema Joshua kwenye tofuti ya Matchroom Boxing.

Joshua, hajawahi kupoteza pambano lolo