#WC2018: Mina: Colombia haikustahili kufungwa

Wednesday July 4 2018

 

By Fadhili Athumani

Moscow, Russia. Baada ya kuibuka shujaa wa muda mfupi, kwa masikitiko makubwa, Yerry Mina, aliishuhudia Colombia yake anayoioenda ikichomolewa na watoto wa Malkia kwa matuta.

Roho ilimuuna sana. Colombia waliondolewa mashindanoni kwa mikwaju ya penalti baada ya kulazimisha sare ya 1-1 kibabe katika dakika za lala salama na sasa Mina, anaamini hawakustahili kufungwa katika mchezo ule wa mwisho wa hatua ya mtoano uliopigwa jana usiku, katika uwanja wa Spartak.

Beki huyo wa Barcelona, amefumania nyavu mara tatu katika michuano hii, ikiwemo bao lililowang'oa Senegal pamoja na bao la kusawazisha dhidi ya England jana usiku na kulazimisha mchezo kuingia dakika 30 za nyongeza.

Hii ni mara ya pili kwa wababe hawa wa Amerika Kusini kupoteza mechi kwa staili kama hii baada ya kung'olewa kwa na Brazil katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, lakini Mina anasema hawakuumia sana kutolewa na Brazil wakati ule kama ilivyo sasa. Beki huyo, anaamini ni aibu kung'olewa na watoto walaini laini wa Malkia.

"Ni pigo kubwa sana. Ni aibu, inaumiza sana. Tulikuwa na uhakika wa kusonga mbele. Baada ya lile bao, tulikuwa tunaiona Sweden mbele yetu na si vinginvyo, hatukustahili kufungwa, kwa jinsi tulivyojituma, kwa namna tulivyopambana, ni ngumu kuamini tumetolewa," alisema Mina.

Mina, mwenye umri wa miaka 23, alisaini kuwatumikia wababe wa Kayalunya, akitokea katika klabu ya Palmeiras mapema mwezi Januari mwaka huu, ambapo mpaka sasa ameshaingia dimbani mara tano. Kiwango alichokionesha kwenye Kombe la Dunia, kimevivutia vilabu vingi, lakini anasema atahitaji muda wa kuamua