Njia rahisi kubaini unene uliokithiri

Kufanya mazoezi na kuushughulisha mwili mara kwa mara katika maisha yetu ya kila siku ni moja ya njia rahisi za kuufanya mwili kuwa imara kiafya.

Mazoezi yanatufanya kuwa na afya bora hivyo kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa ya moyo, kisukari na unene uliokithiri.

Wengi wafanya mazoezi watu wazima huwa na nia ya kukabiliana na unene au uzito uliokithiri kwani hali matatizo ya kiafya katika kundi la Utapiamlo. Ni kawaida watu walio wengi hufanya mazoezi lakini hutajui tuna uzito kiasi gani au kutofahamu unene alio nao mtu upo katika kundi gani la uzito.

Ni muhimu sana kwa mtu yoyote yule hata asiye mfanyaji mazoezi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa uzito wa mwili ili pale unapozidi kiwango cha kawaidi hatua za mapema zichukuliwe.

Kitaalamu zipo njia kadhaa ambazo hutumika kubaini unene uliokithiri au kujua mtawanyiko wa mafuta yaliyorundikana mwilini.

Njia hizo na njia za kimahesabu kwa upimaji wa mzunguko wa kiriba tumbo na kugawa kwa urefu wa mwili hujulikana kama waist circumference ratio.

Njia ya pili ni waist-hip ratio yaani uwiano wa mzunguko wa kiriba tumbo na mzunguko wa paja na ya tatu ni Body Mass Index (BMI) ambayo ni ulinganishaji wa uzito na urefu wa mwili. Njia ya BMI ndio inatumika zaidi kutathimini uzito wa mwili kwa watu wazima, siku ya leo nitaelenga zaidi njia hii kwani ndiyo inatupa taswira ya unene mwilini.

Kwa kawaida hutumia fomula ya kimehasibu kwa kugawa wa uzito katika kilogramu na urefu katika mita kipeuo cha pili. Mfano mtu mwenye Kilo 65 na urefu mita 1.5, BMI ni 70 gawa kwa 1.5 mara 1.5.

Kwa kutumia fomula vipimo vya uzito na urefu zao linalopatikana baada ya kukokotoa ndiyo hujulikana kama BMI, njia hii inatuwezesha kubaini kama ni unene uliokithiri au ni uzito mdogo sana.

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani-WHO BMI inatuwezesha kuanisha uzito wa mtu katika makundi matano. Jibu linalopatikana baada ya kukokotoa ndilo linatoa ainisho la uzito.

Kwa watu wazima BMI ya 18.5-24.9 kitabibu ni uzito salama kiafya, 25.0-29.9 hapa ni uzito mkubwa, 30.0-39.9 hapa huesabika kama ni unene na 40.0 kuendelea ni unene uliokithiri. Endapo BMI itakuwa chini ya 18.5 maana yake ni kuwa mtu huyo ana uzito mdogo sana.

Katika BMI hapa tunaweza kutofautisha uzito uliokithiri, unene na unene uliokithiri hivyo wataalam wa afya huitumia njia hii kutathimini hatari za kiafya wanazoweza kuzipata watu baada ya matokeo ya BMI. Njia hiii ya BMI ni rahisi na haina gharama, ni njia ambayo inawezesha kubaini mrundikano wa mafuta mwilini na uzito uliokithiri kirahisi. Makampuni ya simu za smart wana mfumo laini ndani ya simu wenye kikokotozi cha BMI unachokifanya ni kujaza tu uzito (Kg) wako na urefu wako kisha inakupa majibu (m).

Ingawa BMI si moja kwa moja inapima mrindikano wa mafuta yote mwilini lakini ni kiashiria muhimu kinachotuonyesha kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa yasiyoambukiza.