Sababu za mwasho wa ngozi kipindi cha joto-2

Friday February 8 2019Dk Shita Samwel

Dk Shita Samwel 

Ukiacha hali ya joto iiyopo sasa, leo nitaeleza vitu ambavyo mara kwa mara vinavyochangia kujitokeza hali hiyo.

Nikianza na tatizo la ukavu wa ngozi ambalo kitabibu hujulikana kama Xerosis.Tatizo hili huwa ni matokeo ya vitu vilivyomo katika mazingira ikiwamo hali ya hewa ya joto ay baridi.

Mfano kutumia vitu kama kiyoyozi kwa muda mrefu au kuoga maji vinaweza kuleta ukavu katika ngozi na kuleta mwasho

Sababu ya pili ni maradhi ya ngozi na yale yanayoleta mapele ikiwamo ukurutu, vipele vya tete maji, shambulizi la ngozi na mba/fangasi.

Magonjwa ya ogani za ndani ya mwili ikiwamo kushindwa kufanya kazi kwa ini na figo zinaweza kusababishwa mrundikano wa taka sumu ambazo zinaweza kusababishwa mwili kuwasha. Pia magonjwa kama saratani, VVU na maradhi ya tezi ya shingo yanaweza kuleta mwasho.

Kuathirika kwa mishipa ya fahamu inaweza kusababisha mtu kupata hali ya mwasho, mfano wagonjwa wa kisukari na mkanda wa jeshi huaribu mishipa ya fahamu na kuwafanya wapate hisia za kuwasha.

Vitu kama nguo, kemikali, sabuni tunazoogea, mafuta, krimu, vipodozi na vumbi vinaweza kuleta uchokozi na kusababisha kutokea kwa mzio (allergy). Mzio hutokea baada ya mwili kuchokozwa na kujibu mapigo na kutirisha kemikali zinazosababisha kuwasha.

Baadhi ya dawa za antibiotics, dawa za fangasi, malaria, maumivu zinaweza kuwa na madhara madogo ikiwamo kuleta mwasho na vipele. Hali ya kuwa mjamzito huleta mabadiliko ya kim

wili yanayoweza kuchangia wajawazito kupata mwasho hasa katika maeneo ya tumboni, mikononi, mapajani na katika matiti.

Ni kawaida kabisa kwa baadhi ya wagonjwa sababu ya kuwashwa inaweza isijulikane lakini wakaweza kupona kwa dawa za kawada, na vile vile tatizo hili linaweza kuwa sugu na kudumu mwilini.

Karibia vituo vingi vya afya na hospitali za wilaya zina vitengo vya huduma za magonjwa ya ngozi na magonjwa yanayoenea kwa kujamiiana hivyo unapoona una dalili za mwasho sugu fika katika vituo hivyo kwa ushauri na matibabu.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu