Tumia njia hii kutibu sikoseli

Sikoseli au selimundu ni ugonjwa wa kukauka damu mwilini. Mgonjwa huishivizuri kwa muda fulani tu, ghafla damu inapungua.

Huu ni ugonjwa hatari sana. Watu wengi hupoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa huu.

Katika tiba mbadala tunashauri mgonjwa atumie magome ya mninga ili kujitibu.

Huu ugonjwa unaweza kutibika endapo dawa hiyo asili itatumiwa vizuri pamoja na kufuata ushauri wa mtoa tiba.

Watu wanadhani tiba mbadala haina namna ya kutibu sikoseli.

Watu wenye ugonjwa huu wanaweza kuhitaji kutumia dawa kila siku, hata wakati wanapokuwa na afya njema.

Pia, wanaweza kujisikia vizuri zaidi kama wakifanya mambo yafuatayo.

Kuepuka kukaa sehemu yenye baridi mno au joto kupita kiasi. Wanashauriwa kunywa kunywa maji mengi walau glasi nane kila siku na kula chakula chenye lishe bora.

Pia, wanashauriwa kupumzika vizuri na kulala muda mrefu. Watu wazima wenye sikoseli hawatakiwi kunywa pombe na kuvuta sigara.

Pia, wanashauriwa kuzungumza na daktari kama wakipanga kushika ujauzito.

Watu wenye sikoseli wapelekwe hospitali ya karibu zaidi wakiwa na homa kali, homa ya manjano (ngozi na macho yanakuwa manjano). Pia, wakihisi udhaifu au kushindwa kusogeza sehemu za mwili (kama mkono au mguu), wakipoteza fahamu au kifafa, wapelekwe hospitali.

Tiba ya sikoseli

Ugonjwa huu unaweza kutibika; chukua magome ya mninga kikombe kimoja, tia kwenye maji lita moja.

Chemsha kisha kunywa kikombe kimoja mara tatu kwa siku.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala.