Arusha wapitisha bajeti ya Sh361 bilioni

Friday March 16 2018

 

Arusha. Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha imepitisha bajeti ya Sh361.7 bilioni zitakazotumika mwaka wa fedha 2018/19.

Akiwasilisha mapendekezo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa Arusha, Richard Kwitega alisema Sh247.6 bilioni zitatumika kulipa mishahara ya watumishi na Sh70.1 bilioni zitazoelekezwa kwenye miradi ya ya maendeleo wakati Sh10.3 bilioni ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

“Mkoa unakusudia kupata Sh33.5 bilioni kutoka vyanzo vya ndani ya halmashauri,” alisema Kwitega.

Wakichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mwenzake wa Monduli, Julius Kalanga waliunga mkono bajeti hiyo lakini wakaomba fedha kutoka Serikali Kuu zitumwe kwa wakati.

Lema alishauri kuwapo kwa uhusiano mzuri baina ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanikisha ukusanyaji wa kiwango kilichokusudiwa. (Mussa Juma)

Advertisement