Mwongozo wa Kufanya Maombi ya Kazi Mtandaoni kwa Ufanisi | BrighterMonday

Muktasari:

  • Umeshajiuliza kama unajua kila kinachohitajika ili uweze kuomba kazi mtandaoni kwa ufanisi? CEO wa BrighterMonday Tanzania anaelezea baadhi ya mahitaji hayo hapa.

Maafisa Uajiri sasa wanatumia mifumo ya uchujaji ya mtandaoni ili kupata watu wanofaa kwa nafasi wanazotaka kujaza. Jinsi utakavyo kamilisha utaratibu wa kuomba kuomba kazi mtandaoni mtandaoni ndivyo kutaonyesha ushindani wako katika soko la ajira. CEO wa BrighterMonday Tanzania Mili Rughani ameorodhesha baadhi ya mambo muhimu ya kukumbuka ili uweze kufanikiwa kwenye maombi yako.

Pitia Maelezo ya Kazi

Hakikisha umesoma maelezo yote ya kazi kabla hujaanza utaratibu wa kuomba. Waombaji wengi hufanya kosa la kupitia juujuu tu na kukimbilia kufanya maombi. Maelezo ya kazi yatakujulisha kama una sifa zinazohitajika au la, hivyo usipoteze muda wako maana kama huna sifa basi maombi yako yatakataliwa. Ukisoma kwa umakini utaweza kujua ni sifa zipi za muhimu zinazohitajika, hii itakuwezesha kurekebisha CV yako ili kusisitiza sifa hizi.

Hariri CV Yako

Kazi nyingi zinazotangazwa mtandaoni zinahitaji uweke CV yako wakati wa maombi. Hariri CV yako ili ifae kwa ajili ya kazi unayotaka kupata. Kama unaomba kazi zaidi ya moja hakikisha unaandaa CV tofauti zinazofaa kwa kila moja. Pia, hakikisha maelezo unayoweka kwenye CV yanafanana na yale uliyoweka kwenye barua ya maombi (kama ipo). Baadhi ya mifumo ya usaili inaangalia maelezo ya kwenye CV na kwenye barua ya maombi, hivyo hakikisha hakuna makosa yoyote.

Kama unahitaji, unaweza kuomba ushauri wa kitaalam kutoka kwa Mshauri wa Ajira kuhusu uandaaji wa CV. Kampuni kama BrighterMonday  Tanzania zinaweza kukusadia kwenye hili. Ukiwapatia CV yako, wataalamu wao wataipitia na kukupatia ushauri kwa njia ya barua pepe au simu.

Hariri Wasifu Wako wa Mtandaoni

Baadhi ya makampuni hutaka waombaji kutengeneza wasifu mtandaoni kabla ya kuomba kazi. Wasifu huu huhifadhiwa kwenye rajisi yao na hutumika kwenye usaili kila wanapotangaza kazi. Hakikisha una rekebisha wasifu wako kila wanapotangaza kazi mpya ambayo ina kufaa ili kusisitiza sifa zinazohitajika. Kama umepata ujuzi mpya basi hakikisha unauweka kwenye wasifu wako ili kujiongezea fursa za ajira. Kama umejiunga na kampuni ya uajiri ya mtandaoni, basi watakupatia dondoo mbalimbali zitakazo kueleza jinsi ya kuhariri wasifu wako.

Jitengenezee Mfumo wa Kupata Taarifa

Ukishafanikiwa kufanya maombi ya kazi mtandaoni, hakikisha unafuatilia mchakato wa uajiri. Kama kampuni iliyotangaza ajira ilihitaji utengeneze wasifu mtandaoni, basi watakutumia taarifa kuhusu maombi yako na yalipofikia. Kampuni kamaBrighterMonday zinafanya utaratibu huu. They not only send RSS feeds on your application progress, they will also alert you to new job openings that you qualify. Watakutumia feed za RSS kuhusu maombi yako yalipofikia, pia watakutumia taarifa pale kazi mpya zinazo kufaa zinapo tangazwa. Pamoja na hayo, taarifa hizi zitakujulisha kama kuna maelezo unatakiwa uongeze kwenye maombi yako au kama tangazo la kazi limefungwa. Waombaji wengi hukosa fursa kwa sababu hawakupata taarifa ndani ya muda.

Tafuta Kwenye Maeneo Sahihi

Ili kupata kazi unayotaka, inabidi uwe tayari kuitafuta. Bahati nzuri, unaweza kutafuta kazi ukiwa nyumbani unachohitaji ni kompyuta na intaneti tu. Kuna  makampuni mengi ya uajiri ya mtandaoni ambayo unaweza kujiunga nayo ili uanze kufanya maombi ya kazi. Makampuni haya huwa na rajisi kubwa za matangazo ya kazi kutuoka kwa waajiri mbalimbali. Unaweza kutembelea maonyesho ya ajira, au kupigia simu waajiri mbalimabli na kuuliza kuhusu utaratibu wa kuomba kazi kwenye tovuti zao.

Wasilisha Nyaraka Zako Katika Muundo Ulioelekezwa

Hakikisha unahofadhi nyaraka zako katika muundo ambao unaweza kufunguliwa kwa urahisi na afisa uajiri. kwa MS Word, inashauriwa uhifadhi nyaraka zako kama faili la .doc. Pia unaweza kuhifadhi kama faili la .pdf ili kuzuia lisihaririwe kwa bahati mbaya. Kama nyaraka zako zitapitia hatua nyingi za usaili, muundo wa PDF utasaidia kuhakikisha nyaraka zako hazifanyiwi mabadiliko yoyote.

Jinsi utakavyo kamilisha maombi yako ya kazi ya mtandaoni ndio kutaamua kama utaajiriwa au la. Jiunge na BrighterMonday Tanzania upate dondoo kuhusu maombi ya kazi, uandishi wa kitaalam wa CV, na pia upate rajisi kubwa ya kazi ambazo zinakufaa