Shirika la Ndege Qatar lapunguza bei

Thursday January 11 2018

 

 Mtendaji mkuu wa biashara wa Shirika la Ndege la Qatar, Ehab Amin amesema wameanza mwaka 2018 na punguzo la bei kwa safari za kwenda Mascat, Delhi, London, New York na Guangzhou. Shirika hilo lenye ndege zaidi ya 200 limetangaza nafuu hiyo ya asilimia 30 na ofa nyinginezo kwa wateja hususan kwa safari zitakazopangwa Januari 9 hadi 16. “Wateja watakaopanga safari kupitia tovuti ya shirika wataingia kwenye droo maalumu ambapo 10 watajishindia safari za bure umbali wa maili 100,000 kila mtu na vocha ya hotel ya siku tatu,” alisema. (Ephrahim Bahemu)

Advertisement