Tanga yajivunia vigezo vitatu vya kuongeza ufanisi

Thursday April 12 2018

 

By Burhani Yakub, Mwananchi [email protected]

Tanga. Bandari ya Tanga imeainisha vigezo vitatu vitakavyoiwezesha kuongoza katika kuhudumia shehena kwa haraka kati ya bandari zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Vigezo hivyo ni uwapo katika eneo lenye kufikika kwa urahisi kutoka pande zote duniani; TPA kuanza kuwasilisha vitendea kazi vya kisasa; na Tanga kuwa na shughuli nyingi kutokana na uwekezaji unaofanyika.

Meneja wa TPA Mkoa wa Tanga, Percival Salama alivitaja vigezo hivyo juzi wakati wa uzinduzi wa wiki ya kumbukumbu ya miaka 13 ya huduma za bandari nchini.

Naye mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema katika kuhakikisha upitishaji bidhaa za magendo kupitia bandari bubu unakomeshwa, Serikali imeamua kushirikisha vyombo vyote vya ulinzi kufanya doria badala ya kutegemea polisi pekee.

Advertisement