Total kuosha magari kwa teknolojia mpya

Monday April 16 2018

 

Dar es Salaam. Kampuni ya mafuta ya Total imezindua huduma ya kuosha magari kwa wateja wake.

Mkuu wa kitengo cha mauzo wa Total, Nikesh Mehta alisema huduma hiyo inawalenga wateja wasio na muda mwingi wa kusubiri. “Wateja wataoshewa magari yao kwa muda mfupi baada ya kujaza mafuta na kupata huduma nyingine za kiufundi tunazotoa,” alisema.

Mehta alisema tayari huduma hiyo imepokewa vizuri katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access ambako imeanza kutolewa.

“Kuna sehemu nyingi za kuosha magari lakini huduma hii ni ya kipekee kutokana na utaalamu na teknolojia inayotumika,” alisema.

Mehta alisema wana mpango wa kuanzisha huduma hiyo katika vituo vyake zaidi ya 90 nchini. (Mwandishi Wetu)

Advertisement