Mwinyi ahimiza kilimo cha mazao ya viungo

Thursday July 12 2018

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi. 

By Jackline Masinde, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi amewataka wakulima wa mazao ya viungo nchini kuzalisha kwa wingi ili kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza juzi alipotembelea maonyesho ya biashara ya kimataifa, alisema mazao hayo ikiwamo ndimu, limao, karafuu na mwani yanapotea kila siku licha ya kuwa na faida kubwa kiuchumi na kimwili.

Katika ziara yake hiyo, Rais huyo mstaafu alizindua siku maalumu ya zao la mwani linalolimwa zaidi visiwani Zanzibar.

Alisema amevutiwa na zao hilo linalolimwa zaidi visiwa vya Zanzibar na ni la nne kwa Ukanda wa Afrika Mashariki linalotumika kuzalisha viungo mbalimbali na mafuta ya kula.

Pia, alisema mazao ya mwani, limao na karafuu hayatiliwi mkazo jambo linalosababisha upatikanaji wake kuwa adimu.

Mwinyi pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima wanaozalisha mazao hayo kuzalisha kwa wingi walau tani 23 kwa mwaka .

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Zanzibar, Amina Salum Ally alisema mwani inazalishwa tani 15 hadi 16 kwa mwaka huku watumiaji wa zao hilo wakifikia asilimia 25.

Advertisement