Sirro: Somesheni watoto kujenga jamii iliyoelimika

Thursday July 12 2018Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro 

By Anthony Mayunga

Serengeti. Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amewataka wakazi wa kijiji cha Robanda, kata ya Ikoma wilayani hapa mkoani Mara kuwasomesha watoto kama njia ya kuandaa viongozi wajao.

IGP Sirro alisema hayo juzi akiwa ziarani wilayani hapa na alikutana na kuzungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na askari wa kituo cha Mugumu.

Pia, alikagua nyumba za askari katika kituo kidogo cha polisi Robanda kilichojengwa na kukabidhiwa mwaka jana na kijiji hicho.

Alisema elimu ipewe kipaumbele ili kujenga Taifa la watu walioelimika.

“Sisi akina Sirro tunang’atuka kama hamtasomesha watoto nani atashika nafasi hizi, nawasisitiza sana ndugu zangu wekezeni kwenye elimu,” alisema Sirro.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Mrobanda Japani alisema uamuzi wa kujenga nyumba za askari ni kuhakikisha amani inakuwapo kwa jamii.

Advertisement