11, 800 wapata maji baada ya kusota miaka saba

Wednesday September 11 2019

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Waziri wa Maji nchini Tanzania,  Profesa Makame Mbarawa leo Jumatano Septemba 11,  2019 amezindua mradi wa maji katika mtaa wa Nghong’onha  jijini Dodoma baada ya wananchi wa eneo hilo kuchota maji kwenye makorongo kwa miaka saba.

Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Jiji la Dodoma (Duwasa), David Pallangyo amesema mradi huo utawanufaisha wakazi 11, 800.

Amesema mradi huo utapunguza gharama za ununuzi wa maji kutoka Sh250 hadi Sh25 kwa ndoo yenye ujazo wa lita 20.

“Kabla ya mradi huu wakazi hawa walikuwa wakinunua maji kwa kati ya Sh250 hadi Sh500 kwa ndoo moja ya lita 20,” amesema Pallangyo.

Amesema mradi huo umegharamiwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Advertisement